Anataka kuwacheleweshea watoto matumizi kwa makosa ya mama

Swali: Nimemtaliki mwanamke ambaye tayari tulikuwa tumeshazaa nae. Kila mwezi namtumia yeye na watoto wake matumizi. Lakini ananifanyia tabia mbaya na wala hatumii matumizi hayo vizuri. Je, inajuzu kwangu kumcheleweshea matumizi kwa lengo ka kumtia adabu?

Jibu: Matumizi ni kwa ajili ya watoto wako. Je, unataka kuwaadhibu watoto wako kwa sababu ya mwanamke huyu? Hapana. Matumizi ni kwa ajili ya watoto wako.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (58) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/15-01-1438-ighastat.mp3
  • Imechapishwa: 25/10/2017