Anataka kuwa mjakazi wangu


Swali: Amesema (´Azza wa Jall):

إِنْ هِيَ إِلَّا أَسْمَاءٌ سَمَّيْتُمُوهَا أَنتُمْ وَآبَاؤُكُم مَّا أَنزَلَ اللَّـهُ بِهَا مِن سُلْطَانٍ

“Hayo si chochote isipokuwa ni majina mmeyaita nyinyi na baba zenu wala Allaah hajateremshia dalili yoyote.”[1]

Mwanamke wa kikafiri amekubali kuwa mjakazi wangu. Inafaa kwangu kutangamana naye kwa njia hii?

Jibu: Hapana. Haijuzu kwa mtu kujifanya mtumwa mwenyewe. Nafsi yake sio milki yake. Utumwa hauwi isipokuwa kwa ile njia inayojulikana. Utumwa unakuwa pale ambapo wanawake na watoto wa kikafiri wanapotekwa nyara. Wanatekwa nyara na hawauawi. Wanatekwa nyara kwa ajili ya Jihaad katika njia ya Allaah. Kwa ajili hii wanasema kuwa utumwa ni kule kutokuweza kunakutokamana na ukafiri. Pindi walipokataa kumuabudu Allaah ndipo Allaah akawafanya kuwa watumwa wa waja. Hii ni adhabu kwao. Wamekimbila ule utumwa ambao wameumbwa kwa ajili yake na badala yake wakawa watumwa wa matamanio na shaytwaan.

[1] 53:23

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (71) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah26-07-1438h%20-%20Copy.mp3
  • Imechapishwa: 26/08/2017