Swali: Kila siku nasafari nje ya ar-Riyaadh umbali wa 100 km na narudi mwishoni mwa siku kwa sababu ya masomo. Je, inajuzu kwangu kukusanya Dhuhr na ´Aswr?
Jibu: Ndio. Wewe una haki zaidi ya ruhusa kuliko wengine. Yule ambaye anasafiri kila siku ana haki zaidi ya ruhusa kuliko wengine. Midhali unasafiri 100 km au zaidi, basi wewe ni msafiri.
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (79) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah-9-2-1439-01.mp3
- Imechapishwa: 05/03/2018