Anarudi katika dhambi kila baada ya kutubu

Swali: Ni ipi hukumu kwa mja ambaye kila anapotubu juu ya dhambi baadaye anairudi?

Jibu: Akitubu tawbah ya kweli juu ya dhambi basi atambue kuwa tawbah inafuta yaliyo kabla yake. Akirudi upya basi dhambi zinarudi upya juu ya ile dhambi mpya. Kuhusu ile dhambi ya mwanzo ambayo alitubu tawbah ya kweli amekwishafutiwa. Kila tawbah inafuta yaliyopita kabla yake na kunabaki [dhambi] mpya.

Kwa hiyo ni atilie manani tawbah, alazimiane nayo na ajitahidi kujisalimisha na madhambi. Kuhusu tawbah ni yenye kufuta yaliyo ya kabla yake. Hatochukuliwa hatua kwa ile dhambi ya mwanzo muda wa kuwa ametubu tawbah ya kweli.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaad-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/4297/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D9%85%D9%86-%D9%8A%D8%AA%D9%88%D8%A8-%D9%85%D9%86-%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%B9%D8%B5%D9%8A%D8%A9-%D8%AB%D9%85-%D9%8A%D8%B9%D9%88%D8%AF-%D8%A7%D9%84%D9%8A%D9%87%D8%A7
  • Imechapishwa: 03/07/2020