Swali: Naswali usiku kile kiasi anachokitaka Allaah na napiga Rak´ah nyingi. Natoa Tasliym baada ya Rak´ah tatu na Rak´ah nne mpaka napoteza hesabu nimeswali Rak´ah ngapi. Ni ipi hukumu ya swalah yangu?

Jibu: Ajengee juu ya yakini. Akiwa na dhana kubwa juu ya kitu basi ajengee juu yake kisha asujudu sujuud ya kusahau. Akiwa na dhana kubwa ya zile Rak´ah alizoswali basi hakuna kinachomlazimu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21663/حكم-من-يسهو-كثيرا-فلا-يعلم-كم-صلى
  • Imechapishwa: 08/09/2022