Anapokaa eda mwanamke aliyeachika

Swali: Mwanamke ambaye ana talaka rejea au talaka isiyokuwa rejea kukaa kwake eda daima kunakuwa kwenye nyumba ya mume wake?

Jibu: Mwanamke mwenye talaka rejea anatakiwa kukaa eda kwenye nyumba ya mume wake ikiwepesika kufanya hivo. Isipowepesika anatakiwa kwenda kwa familia yake. Kuhusu mwanamke asiyekuwa na talaka rejea imeharimika. Kwa sababu hazingatiwi tena kuwa mke wa mwanamme huyo. Akimtaliki mara tatu au akajivua katika ndoa basi anatakiwa kutoka. Mwanamke mwenye talaka rejea ule ukaaji wake nyumbani kwake ni miongoni mwa sababu za kumfanya mume kumrejea ikiwa amemtaliki talaka mbili baada ya kumwingilia.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21678/اين-تقضي-المطلقة-عدتها
  • Imechapishwa: 17/09/2022