Anapoenda likizo katika miji ya waislamu anajidhihirisha kuwa ni mwema

Swali 09: Kuna mtu ambaye kupinda kwake kunatambulika na anaishi Marekani. Anapokuja Yemen basi anadhihirisha wema na anatoa pesa katika njia za kheri ilihali mali hizo ni za haramu.

Jibu: Huyu hakuna anachopata isipokuwa tu maneno ya watu. Kuhusu ujira mbele ya Allaah hapati kitu ikiwa anafanya hivo kwa kujionyesha. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

أَلَا لِلَّـهِ الدِّينُ الْخَالِصُ

“Zinduka! Ni ya Allaah pekee dini iliyotakasika.”[1]

وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ

“Hawakuamrishwa jengine isipokuwa wamuabudu Allaah pekee hali ya kumtakasia yeye dini.”[2]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule anayetaka kujionyesha basi Allaah atamfanya kuonekana na yule anayetaka kusikika basi Allaah atamfanya kusikika.”[3]

Hakika mwenye kujionyesha hawezi kuthibiti katika ´ibaadah.

[1] 39:03

[2] 98:05

[3] al-Bukhaariy (6499) na Muslim (93).

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tuhfat-ul-Mujiyb, uk. 60-61
  • Imechapishwa: 29/03/2020