Anapitwa na swalah kwa sababu ya swawm ya Sunnah


Swali: Kuhusiana na funga ya Nabii Daawuud ambapo anafunga siku moja na kufungua siku ya kufuata ni swawm imewekwa katika Shari´ah. Lakini jambo hili likipelekea mtu akaharibu baadhi ya mambo ya wajibu. Je, katika hali hii inakuwa inakubalika Kishari´ah juu yake kama kwa mfano analala wakati wa swalah?

Jibu: Anaharibu mambo ya wajibu kisha anafanya jambo lililopendekezwa? Haijuzu. Anatakiwa kuhifadhi mambo ya wajibu kwanza. Baada ya hapo ndio afanye yale mambo yaliyopendekezwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (88) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/igahssat.mp3
  • Imechapishwa: 18/09/2018