Anapata ujira wa kutembea kwenda msikitini asipohudhurisha nia?


Swali: Kutembea kuiendea swalah msikitini ni jambo lina ujira mkubwa. Je, ni lazima kwa yule mtembeaji ahudhurishe ujira mkubwa juu ya kutembea kwake kwenda msikitini? Akisahau na asihudhurishe jambo hilo pamoja na kutambua kwake ujira, je, kipindi hicho anapata ujira huu?

Jibu: Ndio, bado anapata ujira wake. Akihudhurisha jambo hilo ndio bora. Hilo ni kama mfano wa subira juu ya msiba. Mtu akisubiri juu ya msiba anapata ujira. Akihudhurisha jambo hilo anapata pia ujira mwingine; nao ni ujira wa subira na kutarajia malipo.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (19)
  • Imechapishwa: 12/02/2021