Anapata dhambi ingawa anadai anachonga nyusi kwa kumpambia mume

Swali: Mwanamke anachonga nyusi kwa ajili ya kumpambia mume wake na ni mwenye kuvaa Hijaab na wala haonyeshi mapambo yake isipokuwa kwa mume wake tu. Ni yepi ambayo ni wajibu kwake?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemlaani mwanamke mwenye kuchonga nyusi na mwenye kuchongwa, mwanamke mwenye kutengeneza mwanya na mwenye kutengenezwa na wanamke mwenye kuunganisha nywele na mwenye kuunganishwa. Wanawale aina hii wote kumepokelewa Hadiyth ambazo ni Swahiyh juu ya kuwalaani. Amefanya dhambi ingawa atadai kuwa amefanya hivo kwa sababu ya kumpambia mume wake. Kumpambia mume kunakuwa kwa mambo yaliyohalalishwa na si kwa mambo ya haramu. Mpambie kwa mavazi, harufu nzuri na kwa wanja. Kuhusu yale aliyoharamisha Allaah hayafai. Asijipambe kwa kutengeneza mwanya, kwa kuchonga nyusi zake na wala haifai akajipamba kwa kitu alichoharamisha Allaah katika mambo mengine ambayo hayajuzu kwake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2792/%D9%87%D9%84-%D9%8A%D8%AC%D9%88%D8%B2-%D9%84%D9%84%D9%85%D8%B1%D8%A7%D8%A9-%D8%A7%D9%86-%D8%AA%D8%AA%D9%86%D9%85%D8%B5-%D9%84%D8%B2%D9%88%D8%AC%D9%87%D8%A7
  • Imechapishwa: 11/01/2020