Anaoga janaba akiwa na plasta kwenye donda

Swali: Mwenye kuweka plasta juu ya kidonda na yuko na josho la janaba na akaoga akiwa nayo kisha akaivua na hakupangusa sehemu yake na akaswali – ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Hakuna neno juu yake. Kwa sababu wakati wa kuoga kwake alikuwa na plasta hii. Lakini ni lazima kupitisha mkono wake juu yake ili awe ameipangusa. Akiipangusa basi twahara yake itakuwa imetimia hata kama baadaye ataivua yuko na twahara.

Muulizaji: Lakini hakupangusa juu yake?

Jibu: Ikipitiwa juu yake na maji basi wapo wanachuoni wanaosema kwamba akiosha kile kinachotakiwa kupanguswa basi itamtosheleza kupangusa. Wengine wamesema kwamba haitoshi kuosha kile kinachotakiwa kupanguswa badala ya kukiosha. Wapo wengine ambao wamesema akipitisha mkono juu yake hakuna neno. Vinginevyo hapana. Mfano wa hilo ni kichwa. Kwa mfano mtu anatawadha wudhuu´ wa kawaida ambapo akaweka kichwa chake chini ya bomba mpaka nywele zake zote zikalowa kwa maji na asipitishe mkono wake juu yazo, haisihi. Kwa sababu huyu amefanya kitendo ambacho hakiafikiani na amri ya Allaah na Mtume wake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Atakayefanya kitendo kisichoafikiana na amri yetu basi atarudishiwa mwenyewe.”

Hapa ni pale itakapohusiana na wudhuu´. Ama inapohusiana na kuoga inasihi. Kwa sababu katika kuoga hakuna kitu kinachotakiwa kupanguswa isipokuwa tu bendeji.

Baadhi yao wamesema ikiwa wakati wa kuoga amepitisha mkono wake juu yake inasihi. Wengine wamesema kwamba inasihi moja kwa moja. Lakini lililo salama zaidi ni kwamba ni lazima apanguse kile kinachotakiwa kupanguswa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (68) http://binothaimeen.net/content/1541
  • Imechapishwa: 21/02/2020