Anamwita mke wake ´mama wa waumini`

Swali: Baadhi ya waume wanawaita wake zao wasifu wa ´mama wa waumini`.

Jibu: Hili ni haramu. Si halali kwa yeyote kumwita mke wake mama wa waumini. Muqtadha yake ni kwamba yeye pia ni Nabii. Kwa sababu wanaosifiwa kuwa ni mama wa waumini ni wakeze Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Je, anataka kujifanyia nafasi ya unabii na ajiite kuwa ni Nabii? Ni lazima kwa mtu kuepuka maneno kama haya na amwomba Allaah msamaha kutokana na yaliyopitika kwake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Manaahiy al-Lafdhwiyyah, uk. 23
  • Imechapishwa: 01/07/2022