Anamuuzia mfanyabiashara dhahabu za kale na kununua zengine mpya

Swali: Nikimuuzia mmiliki wa duka dhahabu za zamani na akanipa pesa. Kisha baada ya hapo nikanunua kutoka kwake dhahabu mpya. Je, katika sura hii kuna ubaya?

Jibu: Katika sura hii hakuna ubaya. Mtu anamiliki mapambo ya zamani. Akaja kwa mfanyabiashara na kumuuzia nazo ambapo akampa pesa. Kisha baada ya hapo akanunua kutoka kwake mapambo mapya. Sura hii haina neno na wala haina utatizi wowote.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (57) http://binothaimeen.net/content/1301
  • Imechapishwa: 20/10/2019