Anamkosea mume wake na mzito wa kuomba msamaha

Swali: Baadhi ya nyakati huzungumza vibaya na mume wangu kitu ambacho kinamkasirisha. Matokeo yake ananikata na kunihama. Nashindwa kumwomba msamaha kwa sababu ya kuona hayaa sana. Je, napata dhambi mume wangu akilala ilihali amenikasirikia napata dhambi?

Jibu: Ni lazima kwako kumridhisha mume wako na ujaribu akusamehe kutokana na uliyoyafanya na usiendelee juu ya kosa. Bali jitahidi akuridhie na pengine akasamehe yale yaliyokutokea. Kufnaya hivo ndio bora. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mume atapomwita mke wake kitandani na asije akalala na huku amemkasirikia, basi hulaaniwa na Malaika mpaka kupambazuke.”[1]

Kwa hivyo ni lazima kwa mwanamke kumtii mume wake na kutoenda kinyume naye.

[1] al-Bukhaariy (3237), Abu Daawuud (2141), Ahmad (02/439) na ad-Daarimiy (2228).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/content/أخطئ-على-زوجي-ولا-أعتذر
  • Imechapishwa: 12/06/2022