Analingania na Hizbiyyuun


Swali: Kuna mtu anasema kuwa ni Salafiy lakini analingania pamoja na Hizbiyyuun na wala hatahadharishi nao. Bali anawatahadharisha wanafunzi zake kutokamana na mambo ya Ruduud na anasema kuhusu baadhi ya wanazuoni wa Salafiyyah kwamba wako katika haki lakini usulubu wao ni wa kimakosa. Anatangamana na Hizbiyyuun kwa wingi. Unasemaje juu ya hilo?

Jibu: Huyu ni mjinga. Huyu ni mjinga. Huyu ameghuriwa. Huyu ni masikini. Huyu si Salafiy. Anawatumikia watu wa batili. Ruduud ni aina fulani ya kuamrisha mema na kukataza maovu. Anasemaje juu ya maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):

كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ

“Mmekuwa Ummah bora uliotolewa kwa watu; mnaamrisha mema na mnakataza maovu na mnamwamini Allaah.”[1]

Ni vipi wamekuwa Ummah bora? Je, si ni kutokana na sifa hizi? Kuamrisha mema, kukataza maovu na kumwamini Allaah. Kuamrisha mema na kukataza maovu kumejengeka juu ya kumwamini Allaah. Ni nini maana ya kumwamini Allaah? Kuamini Kitabu Chake na kutambua ile haki iliyomo na kutambua Sunnah na ile haki iliyomo. [Sauti haiko wazi] Je, mtu anaweza kusema kuwa haifai kuamrisha mema na kukataza maovu? Je, mtu anaweza kusema kuwa yule mwenye kuamrisha mema na kukataza maovu ni mtu wa batili? Je, ´Aqiydah yake si sahihi? Vipi basi tunaweza kusema kuwa Ruduud hazijuzu, ni batili na mfano wa hayo ikiwa tunasema kuwa yule mwenye kuamrisha mema na kukataza maovu yuko katika haki na ni lazima asapotiwe? Yule mwenye kusema hivi basi yeye mwenyewe ndiye mtu wa batili.

[1] 03:110

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://ar.alnahj.net/audio/1531
  • Imechapishwa: 19/06/2021