Anakula vitungu saumu na vitungu maji ili akwepe kuswali msikitini

Swali: Je, makatazo ya kuja kuswali msikitini kwa yule aliyekula kitungu saumu au kitungu maji ni kwa lengo la kumtia adabu? Inafaa kwake kula ikiwa hakukusudia kuacha kuswali pamoja na mkusanyiko japokuwa atakuwa si mwenye kukariri jambo hilo?

Jibu: Ikiwa anakula kitungu saumu au kitungu maji kwa lengo aweze kukwepa swalah kwa mkusanyiko anapata dhambi. Ama akivila kwa haja, amelazimika au kwa sababu ya matibabu hakuna neno. Baadaye akajaribu kuondosha ile harufu yake. Isipoondoka ile harufu yake basi aswali nyumbani kwake na wala asende kuswali na mkusanyiko. Ni mwenye udhuru. Ama akivila kwa ajili ya kukwepa swalah ya mkusanyiko anapata dhambi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (11) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191491#219817
  • Imechapishwa: 04/08/2019