Swali: Je, kuwatukana Malaika ni kufuru inayomtoa mtu nje ya Uislamu?

Jibu: Ndio. Anayemtukana mmoja katika Malaika au mmoja katika Mitume kunahesabika ni kuritadi kutoka katika Uislamu. Nguzo za imani ni kumuamini Allaah, Malaika wake, Vitabu vyake, Mitume wake, siku ya Mwisho na kuamini Qadaar kheri na shari yake. Hizi ndio nguzo za imani. Katika hayo kunaingia vilevile kuwaamini Malaika (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam). Anayewatukana anakuwa mwenye kuritadi. Amesema (Ta´ala):

قُلْ مَن كَانَ عَدُوًّا لِّجِبْرِيلَ فَإِنَّهُ نَزَّلَهُ عَلَىٰ قَلْبِكَ بِإِذْنِ اللَّـهِ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ

“Sema: “Yeyote aliyekuwa adui wa Jibriyl, basi hakika yeye ameiteremsha kwenye moyo wako kwa idhini ya Allaah inayosadikisha yaliyo kabla yake.” (02:97)

Mpaka alipofikia kusema:

مَن كَانَ عَدُوًّا لِّلَّـهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَرُسُلِهِ وَجِبْرِيلَ وَمِيكَالَ فَإِنَّ اللَّـهَ عَدُوٌّ لِّلْكَافِرِينَ

“Yeyote aliyekuwa adui wa Allaah na Malaika Wake na Mtume Wake na Jibriyl na Miykaala, basi hakika Allaah ni adui kwa makafiri.” (02:98)

Amewaita kuwa ni makafiri. Ni dalili inayofahamisha kwamba anayewachukia Malaika au baadhi yao ni kafiri. Mayahudi wanamchukia Jibriyl (´alayhis-Salaam) na wanasema kwamba Jibiriyl ndiye adui wao. Allaah akawajibu namna hii na anawahukumu ukafiri kwa sababu ya kumchukia kwao Jibriyl (´alayhis-Swalaatu was-Salaam).

Wapo pia wanaosema kuwa Jibiryl alifanya khiyana ya amana na kwamba utume ulikuwa unatakiwa kwenda kwa ´Aliy na kwamba eti Jibriyl alifanya khiyana na badala yake akampa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wanasema kwamba mwaminifu alifanya khiyana. Huku ni kumkufuru Allaah (´Azza wa Jall).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam https://ajurry.com/safrawy/chorohat-elakida/chorohat-nawakid-elislam/charh-salah-fawzan/04.mp3
  • Imechapishwa: 01/12/2018