Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kusema kwamba yeye ni kafiri na mshirikina?

Jibu: Akiyasema haya na huku anaamini hivo basi anakufuru. Ama kama amesema hivo pasi na kuamini hivo, bali amesema kwa sababu ya hasira, harudi katika Uislamu hali ya kusalimika. Hivo ndivo alivosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mwenye kusema kwamba ni myahudi au mnaswara. Akiwa anamaanisha kweli basi yeye yuko hivo. Ama akiwa ni mwongo, basi harudi katika Uislamu hali ya kusalimika.”

Haijuzu kutamka mfano wa maneno kama haya.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam http://ajurry.com/safrawy/chorohat-elakida/chorohat-nawakid-elislam/charh-salah-fawzan/03.mp3
  • Imechapishwa: 24/02/2019