Anahisi kutokwa na madhiy wakati wa swalah


Swali: Mimi ni mwanamme ninayetokwa na madhiy sana. Wakati mwingine hutawadha na nikaingia ndani ya swalah na nikahisi madhiy kwenye nguo yangu; wakati fulani inakuwa kabla ya swalah, wakati mwingine baada yake na wakati mwingine katikati ya swalah. Ni ipi hukumu ya madhiy haya kwenye nguo yangu? Nifanye nini yakiwa ni mengi na jambo hilo linakariri?

Jibu: Ukihisi madhiy basi ni wajibu kwako kukata swalah yako pale utapokuwa na dhana yenye nguvu. Kwa sharti isiwe ni wasiwasi. Utapoyakinisha kuwa umetokwa na madhiy basi ni wajibu kwako kurudi na kuosha dhakari. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Osha dhakari yako na uke wako.”

Anatakiwa atawadhe na airudi swalah yake.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (05) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191110#219240
  • Imechapishwa: 20/10/2018