Swali: Ni ipi hukumu kwa mtu ambaye anafunga Ramadhaan na ananuia pamoja nayo swawm ya nadhiri?

Jibu: Hili halijuzu. Anatakiwa kufunga kila moja kivyake. Aanze kufunga Ramadhaan kisha ndio afunge nadhiri. Isipokuwa tu ikiwa kama wakati wa kuweka nadhiri alisema “Allaah ana nadhiri juu yangu kufunga Ramadhaan”. Ameweka nadhiri ya kutekeleza kitu cha wajibu kwa mujibu wa msingi wa Shari?ah. Kwa hivyo hii sio nadhiri. Kwa msingi wa Shari?ah ni nguzo moja wapo ya Uislamu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaam al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14891
  • Imechapishwa: 28/05/2017