Anafuata maoni ya mwanachuoni fulani kwamba mambo ya kuigiza yanafaa

Swali: Ni ipi hukumu ya mtu ambaye anafuata maoni ya mwanachuoni fulani aliyesema kuwa kitu fulani kinafaa. Kwa mfano mambo ya kuigiza. Hebu tuchukulie kuwa mimi naona kuwa mambo ya kuigiza ni uzushi na huyo mtu mwingine amekubali maoni ya huyo mwanachuoni mkubwa anayejuzisha. Je, inafaa kwangu kutukana mfumo wa mtu huyu na kusema kuwa mtu huyu anafuata mfumo wa al-Ikhwaan al-Muslimuun katika jambo fulani au nikamtia katika Bid´ah? Aidha itambulike kuwa mtu huyo ni mwenye kufuata kichwa mchunga.

al-Albaaniy: Je, inafaa kwa mwanachuoni kusema kitu juu ya yule ambaye ameenda kinyume naye?

Muulizaji: Hapana.

al-Albaaniy: Bali vivyo hivyo bali zaidi ya hivo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (778)
  • Imechapishwa: 09/01/2021