Anadhihirisha Uislamu katika nchi ya makafiri

Swali: Ni kipi kidhibiti cha kudhihirisha dini katika miji ya makafiri? Je, maana yake ni kwamba wanawaacha wakaswali na kufunga?

Jibu: Hapana, ni kosa. Baadhi ya watu wanadhani kwamba maana yake ni kule kuwaacha wakaswali na kufunga na hawawasumbui. Haya yapo hata Israaiyl hawawazuii kuswali na kufunga. Kudhihirisha dini sio huku. Kudhihirisha dini ni kulingania kwa Allaah na kubainisha ubatilifu wa shirki na uwajibu wa Tawhiyd. Kwa msemo mwingine ni kwamba analingania katika ´Aqiydah yake. Huku ndio kudhihirisha dini. Kadhalika alinganie katika swalah yake kwa wakati wake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (50) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Umdah%20Fiqh-06-05-1437.mp3
  • Imechapishwa: 09/03/2019