Anachosema mtu wakati muadhini anaposema “as-Swalaatu khayrun minan-Nawm”

Swali: Nikitaka kumuiga muadhini katika adhaana ya al-Fajr na akafika katika kauli “as-Swalaatu khayrun minan-Nawm”, aseme hivo hivo au kuna msemo mwingine wa kusema?

Jibu: Hapana, aseme kama anavyosema muadhini na asiseme kinyume isipokuwa wakati wa “Haiyyaa… “ mbili tu. Mbali na hizi mbili aseme kama anavyosema muadhini, bi maana aseme “as-Swalaatu khayrun minan-Nawm” kama alivyosema muadhini. Isipokuwa kwa dalili inayoonesha umaalum. Na hii ndio Fatwa aliyotoa Shaykh Ibn (Raahimahu Allaah) ya kwamba aseme “as-Swalaatu khayrun minan-Nawm” kama alivyosema muadhini kutokana na ujumla wa Hadiyth:

“Aseme kama anavyosema.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (31) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1431-10-10.mp3
  • Imechapishwa: 15/11/2014