Swali: Hii leo katika jamii za Kiislamu kumeenea kitu kinachoitwa “Anaashiyd za Kiislamu”. Anaashiyd hizi ziko ambazo zina taathira ya sauti kwa mdomo, zengine wanaimba kundi la wanaume ambao wanaimba kwa kurudiarudia kwa sauti ya pamoja, zengine zinatumia ala za muziki na zengine zinatumia dufu. Ni ipi hukumu yazo kwa hali zake zote?

Jibu: Zinatofautiana na haziko katika kiwango kimoja. Anaashiyd ambazo zinatumia muziki na dufu ni mbaya na khatari zaidi. Kutumia sauti na lengo lao kubwa ikawa ni sauti, kupendezesha sauti na sauti isikiwe ni jambo pia ambalo si zuri. Lengo kubwa la mtu inakuwa apendeze sauti, midundo na hafikirii wala hatilii manani ile maana. Lililo la wajibu kwa mtu afanye jambo litalomletea kheri. Badaya Anaashiyd hizi asome Kitabu cha Allaah, Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na asome mneno ya wanachuoni. Asiishughulishe nafsi yake kwa mfano wa Anaashiyd hizi zilizowashughulisha watu kutokamana na kitu ambacho walitakiwa wawe juu yake kuliko kujishughulisha na Qur-aan na Hadiyth.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bid´at-ul-Mawaalid wa mahabbat-in-Nabiyy http://www.ajurry.com/vb/showthread.php?t=36078
  • Imechapishwa: 10/11/2019