Swali: Kuna mwanamke ameamka kutoka usingizini karibu na mida ya adhuhuri na alikuwa hakunuia kufunga kabla ya kulala. Ndipo akafunga siku hiyo hali ya kulipa deni lake la Ramadhaan. Je, ni sahihi?

Jibu: Hapana. Swawm ya faradhi haisihi mpaka mtu anuie kabla ya kwenda kulala, ni mamoja ni Ramadhaan, swawm ya kulipa, kafara au nadhiri. Ama swawm ya sunnah ni sawa kwa mtu akaweka nia wakati wa mchana kwa sharti mtu asiwe alikunywa au alikula baada ya alfajiri kuingia.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (17) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdtf-08011435.mp3
  • Imechapishwa: 01/11/2019