Anaacha kuoa kwa kuchelea kutotimiza haki za wazazi

Swali: Nataka kuoa lakini naacha kufanya hivo kwa kuchelea kutowatendea wema wazazi wangu. Nifanye nini?

Jibu: Ni kosa. Nasema hivi oa. Huenda kuoa kwako ikawa ni sababu ya kuwatendea wema wazazi. Kwa sababu ukioa umeoa kwa sababu ya amri ya Allaah. Matendo mema ni mambo yenye kuvutana. Hivyo oa na harakisha kuoa. Pengine kuoa kwako ikawa ni katika kuwatendea wema ili mwanamke huyo akaja kuwahudumia wazazi wako. Hata kama mwanamke kuwahudumia wazazi wa mume sio wajibu, lakini ni jambo linaingia katika tabia njema. Huenda Allaah akamfanyia wepesi kuwahudumia wazazi hawa wawili.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (55) http://binothaimeen.net/content/1253
  • Imechapishwa: 26/09/2019