Anaacha fatwa za wanachuoni


Swali: Mtu mwenye kujua haki kupitia fatwa za wanachuoni wenye kuzingatiwa kisha akaziacha na kuchukua maneno ya watu waliokurupuka juu ya fatwa. Je, anazingatiwa anawafanya waungu?

Jibu: Hapana shaka. Ikiwa anajua kuwa wako makosani na akayafanyia propaganda maneno yao kwa ajili ya lengo fulani ima kwa ajili ya tamaa ya kidunia, kuificha haki au kuwakhalifu wale wanaofuata haki, hapana shaka kwamba amewafanya ni waungu badala ya Allaah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.alfawzan.af.org.sa/ar/node/2896
  • Imechapishwa: 26/04/2019