Swali: Yale ambayo hii leo yanaitwa kuwa ni “Anaashiyd za Kiislamu” ni katika dini ya Suufiyyah? Tukisema hivo ni aina moja wapo ya kutoka nje ya Shari´ah ya Kiislamu?

Jibu: Yule mwenye kudai kwamba Anaashiyd ni njia moja wapo ya Da´wah na kwamba ni katika dini ana ufanano fulani na Suufiyyah. Kwa sababu Suufiyyah ndio wenye kufanya Anaashiyd katika kumdhukuru Allaah (´Azza wa Jall) na wanajikurubisha kwazo kwa Allaah (´Azza wa Jall). Mwenye kusema kwamba Anaashiyd ni katika Uislamu au ni katika dini ana ufanano fulani na Suufiyyah. Vilevile kuna aina fulani ya kutoka nje ya Shari´ah. Ni aina. Si kwamba  ametoka kikamilifu na kwamba anakufuru. Kwa sababu ameingiza ndani yake kitu kisichokuwa ndani yake. Kuna aina fulani ya kutoka katika Shari´ah. Anaashiyd ni miongoni mwa nyimbo. Ni katika pumbao. Hazifai.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam (09) http://ajurry.com/safrawy/chorohat-elakida/chorohat-nawakid-elislam/charh-salah-fawzan/09.mp3
  • Imechapishwa: 29/03/2019