Swali: Kipi natakiwa kufanya ikiwa nilikuwa na mfanya kazi anayefanya kazi kwangu na nikawa na kiwango cha pesa na sikumpata ili nimkabidhi haki yake?

Jibu: Ikiwa mtu yuko na haki ya mwengine na hakumpata na wala hajui alipo amtolee swadaqah kwa kumnuilia. Allaah atamfikishia nayo. Dhimma yako imetakasika kwa kufanya hivo. Akijitokeza baada ya kipindi fulani akiiomba, basi utampa khiyari; akitaka atakubali swadaqah na atakuwa ni mwenye kupata thawabu na akitaka utampa haki yake na thawabu zitakuwa zako wewe.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaad-ud-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/4428/%D9%85%D8%A7-%D8%AD%D9%83%D9%85-%D9%85%D9%86-%D8%B9%D9%86%D8%AF%D9%87-%D8%AD%D9%82-%D9%84%D8%A7%D9%86%D8%B3%D8%A7%D9%86-%D9%81%D9%84%D9%85-%D9%8A%D8%AC%D8%AF%D9%87
  • Imechapishwa: 18/09/2020