an-Najmiy kuhusu kukusanya Maghrib na ´Ishaa wakati wa majira ya joto

Swali: Muulizaji kutoka Uholanzi anasema kwamba ule msitari mwekundu angani unapotea inapofika nusu ya usiku katika majira ya joto ambapo wanalazimika kubaki macho ili waweze kuswali ´Ishaa kwa mkusanyiko. Je, inafaa kuswali Maghrib na ´Ishaa katika kipindi cha swalah ya Maghrib?

Jibu: Hapana. Hapana.

Swali: Au tuweke saa moja na nusu kati ya swalah hizo mbili, kama tulivyozowea kufanya? Baadhi ya ndugu wamesema kuwa wamemsikia mwanachuoni mmoja Shaykh aliyesema hivo.

Jibu: Mimi siwezi kutoa fatwa juu ya hilo. Saa moja na nusu inatumiwa mahali ambapo msitari mwekundu huyo unapotea baada ya wakati huo. Mtu hawezi kujuzisha kufaa kuiswali ´Ishaa ikiwa msitari mwekundu unapotea kwa kuchelewa zaidi ya hivo. Inaonekana kwamba nyusiku zao huko ni fupi mno.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.al-amen.com/vb/showthread.php?t=8630
  • Imechapishwa: 06/06/2020