Amfuate imamu au akamilishe swalah yake kivyake?

Swali: Yule ambaye amekuja amechelewa akiswali na imamu. Wakati imamu alipoleta Tasliym yule mswaliji akasimama ili akamilishe swalah yake. Kisha baadaye ikaja kubainika kuwa imamu ametoa Tasliym kabla ya kukamilisha swalah yake na hivyo imamu akasimama ili aweze kukamilisha swalah yake. Ni kipi afanye yule mswaliji?

Jibu: Hakuna neno akirudi na akaswali naye. Anapewa udhuru kwa kule kusimama kwake. Vivyo hivyo ni sawa endapo atakamilisha swalah yake na akakamilisha kuswali kivyake. Kwa msemo mwingine ni kwamba yuko na khiyari [kati ya hayo mawili].

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (19)
  • Imechapishwa: 12/03/2021