Ameweka nadhiri ya kufunga Rajab na kuchinja


Swali: Mwanamke huyu ameweka nadhiri ya kufunga masiku kumi ya mwezi wa Rajab katika kila mwaka pamoja na kuchinja kondoo ambaye hakumlenga ni wa aina gani. Akawa amefunga miaka kumi na moja na akachinja kondoo mmoja, akatoa swadaqah miaka ishirini. Hivi anauliza ni kipi kilicho cha wajibu juu yake. Je, inatosha kwake kutoa swadaqah juu ya yale masiku ambayo hakufunga au ni lazima kufunga na kuchinja? Je, inajuzu kwake na kwa familia yake kula katika kichinjwa hicho au hapana? Nataraji kupata faida Allaah akujazeni kheri.

Jibu: Kuweka nadhiri katika mwezi wa Rajab na kuweka nadhiri ya kuipwekesha au kuipwekesha siku maalum kwa ajili ya kufunga ni jambo limechukizwa. Kwa sababu ni katika mambo ya kipindi kabla ya kuja Uislamu.

Kwa hivyo ni wajibu kwa dada muulizaji kutoa kafara ya yamini badala ya kuchinja na kufunga masiku. Kafara yenyewe ni ima kuacha mtumwa huru kulisha masikini kumi ambapo kila masikini atapewa takriban 1,5 kg katika chakula kinacholiwa katika mji au kuwavisha. Asipoweza chochote katika hayo yaliyotajwa basi atafunga siku tatu.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alifta.net/Fatawa/FatawaChapters.aspx?languagename=ar&View=Page&PageID=333&PageNo=1&BookID=12
  • Imechapishwa: 20/03/2018