Swali: Wakati nilipokuwa natawadha nilisahau kupangusa kichwa na nikaosha miguu yangu. Je, ni lazima kurudi kutawadha kikamilifu au nirudi kufuta kichwa kisha nioshe miguu yangu baad ya hapo?
Jibu: Ni lazima kwako kurudi kupangusa kichwa na masikio yako kisha uoshe miguu yako ukiyakumbuka hayo kabla ya kupita kitambo kirefu. Kukipita kitambo kirefu basi unalazimika kutawadha upya. Kwa sababu Muwaalaah[1] ni faradhi miongoni mwa faradhi za wudhuu´.
[1] Tazama http://firqatunnajia.com/06-faradhi-za-wudhuu/
- Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/103)
- Imechapishwa: 12/08/2021