Ameuliwa wakati alipokuwa akitetea heshima ya mwanamke

Swali: Vipi ikiwa mtu atauliwa kwa kutetea heshima ya mwanamke wa Kiislamu?

Jibu: Hapana sahaka kuwa ni shahidi kwa sababu amedhulumiwa.

Swali: Hata kama atauliwa?

Jibu: Muuaji ni mwenye kudhulumu na ataingiaMotoni. Dhalimu ni mwenye kukiuka heshima za waislamu. Ni dhalimu. Kunakhofiwa juu yake kuingia Motoni na yuko chini ya utashi wa Allaah.

Swali: Endapo atamuua kwa ajili ya kumtetea yule mwanamke?

Jibu: Muuaji ni mwenye kujitahidi na mwenye kulipwa thawabu. Muuliwaji ambaye alikuwa anajaribu kuyaendea machafu anastahiki kuingia Motoni – kama ilivyopokelewa katika Hadiyth – kutokana na dhuluma yake. Tunamuomba Allaah usalama.

Swali: Vipi ikiwa mshambuliaji huyo anaweza kuzuiwa bila kuuliwa?

Jibu: Anatakiwa kumzuia kwa njia nyepesi zaidi. Njia hiyo ni kama kumpiga na kumtisha kwa maneno. Ikiwa hazuiliki isipokuwa kwa kuuliwa basi atauliwa:

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

”Basi mcheni Allaah muwezavyo.”[1]

[1] 64:16

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22934/حكم-من-قتل-وهو-يدافع-عن-عرض-امراة
  • Imechapishwa: 18/09/2023