Swali: Siku moja nilipokuwa nachunga kondoo kwa baba yangu katika siku miongoni mwa siku za Ramadhaan iliyobarikiwa alinikabili msichana ambaye na yeye pia anachunga kondoo. Ilikuwa ni kati ya Dhuhr na ´Aswr. Nikaketi pamoja naye na nikaanza kuzungumza naye mpaka hali ikafikia kufanya naye mzaha na kufanya naye romantiki katika siku hiyo ambayo ni ya Ramadhaan. Yakanifika yakunifika pasi na kumjamii msichana huyu. Anauliza hukumu ya kufanya kitu kama hicho mchana wa Ramadhaan?

Jibu: Upande wa hukumu ni kitu kischojuzu. Kwa sababu mwanamke huyu ni wa kando na haifai kwake kuzungumza naye mazungumzo ya kuamsha matamanio. Isitoshe pengine jambo hilo likakupelekea katika fitina na uzinzi. Ni lazima kujichunga na jambo hilo. Kuhusu maongezi ya kawaida ambayo ndani hayana dhambi wala hakuna kinachopelekea katika machafu. Kwa mfano kumuuliza kuhusu hali yake, malisho mazuri, maji na mfano wa hayo ambayo hakuna kitu kinachopelekea fitina hakuna neno.

Kuhusu kufanya mambo ya romantiki na mambo ambayo yanahusiana na machafu, kupelekea katika uzinzi na kusababisha kutumbukia katika madhambi, yote hayo hayajuzu.

Ama kuhusiana na funga yake ni sahihi ikiwa hakutokwa na manii.

Mwendesha kipindi: Ametaja kuwa ametokwa na manii.

Ibn Baaz: Akiwa ametokwa na manii basi ni lazima kwake kulipa siku hiyo. Anapaswa kufungua siku hiyo kwa sababu amefungua kwa kule kutokwa na manii.

Kuhusu madhiy hayafunguzi kwa mujibu wa maoni sahihi zaidi. Madhiy ni majimaji yanayonatanata ambayo yanatoka wakati wa kuamka kwa matamanio. Majimaji haya hayaharibu swawm kwa mujibu wa maoni sahihi zaidi ya wanachuoni.

Ama manii yanaharibu swawm yake na ni lazima kwake kulipa siku hiyo.

Mwendesha kipindi: Lakini halazimiki kutoa kafara?

Ibn Baaz: Hahitajii kutoa kafara. Kafara ni kwa ajili ya jimaa peke yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb https://binbaz.org.sa/fatwas/28366/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D9%85%D8%AF%D8%A7%D8%B9%D8%A8%D8%A9-%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%B1%D8%A7%D8%A9-%D8%A7%D9%84%D8%A7%D8%AC%D9%86%D8%A8%D9%8A%D8%A9-%D9%81%D9%8A-%D9%86%D9%87%D8%A7%D8%B1-%D8%B1%D9%85%D8%B6%D8%A7%D9%86
  • Imechapishwa: 03/05/2020