Ametilia shaka kuzama kwa jua na kuchomoza kwa alfajiri

Swali: Ni ip hukumu ya mwenye kula, kunywa au kufanya jimaa hali ya kutilia shaka kwamba jua limekwishazama au alfajiri haijaingia?

Jibu: Maoni ya sawa ni kwamba analazimika kulipa. Kama alifanya jimaa analazimika vilevile kutoa kafara kwa mujibu wa wanachuoni wengi. Yote haya ni kwa ajili ya kufunga njia watu wasije kuchukulia wepesi na ni salama zaidi kwa ajili ya funga.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tuhfat-ul-Ikhwaan, uk. 180
  • Imechapishwa: 02/06/2019