Swali: Kuna mtu alikuwa mgonjwa hospitalini katika masiku ya Ramadhaan. Alikula daku ili afunge. Lakini baada ya kula daku akatapita ambapo akadangana afunge au asifunge. Kwa msemo mwingine ni kwamba akawa hana uhakika juu ya nia ya funga yake. Lakini baada ya hapo akafunga. Ni ipi hukumu ya swawm yake hii ilihali alikuwa si mwenye uhakika juu ya nia yake mwanzoni mwa siku hiyo kama atafunga au hafungi?

Jibu: Midhali huyu amenuia kufunga lakini akawa na mashaka kama matapishi haya yanaharibu swawm au hayaharibu kisha akaendelea juu ya maazimio yake ya kufunga, swawm yake ni sahihi. Kwa sababu mashaka haya yanatokana na kwamba huku kutapika kunafunguza au hakufunguzi, hakutilia mashaka juu ya nia. Alichofanya ni kutilia mashaka kama matapishi haya yanaharibu swawm au hayaharibu. Tunasema kuwa swawm yake ni sahihi na halazimiki kulipa.

Lakini itambulike kuwa kutapika hakuharibu swawm isipokuwa pale ambapo mtu atajitapisha. Lakini midhali mtu hakukusudia kufanya hivo swawm yake haiharibiki kwa kutapika. Hata kmaa tutasema kuwa mtu hakufanya majaribio yoyote ya kuyazuia matapishi, bali aliyaacha – hakujikokoa na hakuzuia – yakatoka, swawm yake ni sahihi. Kujengea juu ya hili tunamwambia ndugu muulizaji kwamba swawm yake ni sahihi na wala halazimiki kulipa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: l-Liqaa´ ash-Shahriy (42) http://binothaimeen.net/content/942
  • Imechapishwa: 08/05/2018