Ametaka kuswali ´Ishaa lakini amekumbuka hajaswali Maghrib

Swali: Afanye nini mtu aliyeingia msikitini kwa ajili ya swalah ya ´Ishaa kisha akakumbuka kuwa hajaswali Magrhib?

Jibu: Ukiingia msikitini kuswali ´Ishaa kisha ukakumbuka kuwa hujaswali Maghrib, jiunge pamoja na mkusanyiko kwa nia ya swalah ya Maghrib. Imamu ataposimama katika Rak´ah ya nne wewe keti chini katika ile Rak´ah ya tatu ukimsubiri imamu kisha utoe salamu pamoja naye. Una ruhusa pia ya kutoa salamu kisha ukajiunga na imamu katika yale yatayokuwa yamebaki katika swalah ya ´Ishaa.

Kule kutofautiana kwa nia kati ya imamu na mswaliji ni kitu kisichodhuru kwa mujibu wa maoni sahihi zaidi ya wanachuoni. Ni sawa pia ukiswali Maghrib peke yako kisha ukaswali pamoja na mkusanyiko katika yale utayokuwa umewahi katika swalah ya ´Ishaa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Arkaan-il-Islaam, uk. 291
  • Imechapishwa: 03/05/2020