Ameswalisha imamu asiyekuwa mteule

Swali: Muadhini au mswaliji mwingine akiwaongoza watu kabla ya muda wa Iqaamah uliotangazwa kisha akaingia imamu baada ya kumalizika swalah – je, imamu ana haki ya kurudia swalah na kwa nini?

Jibu: Wanazuoni (Rahimahumu Allaah) wamesema kuwa ni haramu kutekeleza swalah kabla ya imamu mteule isipokuwa ikiwa imamu atawapa idhini au akawa na udhuru. Akiwaidhinisha au imamu akafikwa na udhuru na hivyo akachelewa kutokamana na ule muda uliozoeleka na isitoshe uchelewaji huo ukawadhuru maamuma, basi inafaa akatangulia mbele ambaye atawaswalisha. Kwa hivyo, ikiwa muadhini anatambua idhini ya imamu au anajua kuwa ule muda wa kukimiwa swalah umechelewa sana na hivyo akatangulia mbele na kuswalisha, hakuna vibaya. Akitangulia mbele kabla ya wakati wa Iqaamah na akawaswalisha maamuma na swalah ikamalizika, basi bora kwa imamu ni yeye kuwakubalia kitendo chao hicho. Haitakikani kwake kuwaswalisha mwanzo. Bali awakubalie juu ya kitendo hicho. Licha ya kwamba ni lazima kwa wote kumcha Allaah na wasimtangulie imamu isipokuwa kwa udhuru unaokubalika katika Shari´ah.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/content/حكم-صلاة-من-أم-الناس-غير-الإمام-الراتب-في-الصلاة
  • Imechapishwa: 12/06/2022