Ameswali nyuma ya imamu kwa kuketi chini bila ya udhuru

Swali: Nilikuwa naswali nyuma ya imamu kisha mtoto wangu akalia sana kiasi cha kuwashawishi waswaliji. Nikalazimika kuswali hali ya kuketi chini Rak´ah mbili. Baada ya kumaliza kuswali mmoja katika waswaliji akanishauri kuirudi swalah yangu kwa sababu nimemkhalifu imamu. Je, aliyosema ni sahihi?

Jibu: Ndio. Mwenye kuketi chini katika swalah ya faradhi ilihali anaweza kusimama swalah yake inaharibika. Ni lazima kwako kuirudi tena. Hata kama mtoto atalia mwache alie na hakuna neno.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ad-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/3712/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D9%85%D9%86-%D8%B5%D9%84%D9%89-%D8%AC%D8%A7%D9%84%D8%B3%D8%A7-%D8%AE%D9%84%D9%81-%D8%A7%D9%84%D8%A7%D9%85%D8%A7%D9%85-%D8%AF%D9%88%D9%86-%D8%B9%D8%B0%D8%B1
  • Imechapishwa: 13/03/2020