Ameswali miaka mingi bila ya wudhuu´


Swali: Niliswali Swalah nyingi ambazo sijui idadi yake bila ya kuwa na twahara na nilifanya hivo kwa kukusudia na kwenye miaka mbali mbali na leo nimetubu. Kipi kinachonilazimu kwa hali yangu kama hii?

Jibu: Ikiwa ulikusudia kuswali bila ya kuwa na wudhuu, wewe ni kama aliyeacha Swalah kwa kukusudia. Mwenye kuacha Swalah kwa kukusudia ni kafiri. Maadamu umetubu kwa Allaah na umeingia katika Uislamu upya, ni juu yako kuhifadhi Swalah. Tawbah inafuta yaliyo kabla yake. Tawbah sahihi inafuta yaliyo kabla yake. Hifadhi Swalah baada ya kutubu na Allaah Anasamehe yaliyopita.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-is-Saffaariniyyah (07) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/sfranih_07.mp3
  • Imechapishwa: 26/06/2018