Ameswali kwenye msikiti wa kaburi kwa miaka kumi

Swali: Nilikuwa nikiswali kwenye msikiti ulio na kaburi kwa muda wa miaka kumi. Ni ipi hukumu ya swalah zangu kwa muda huu?

Jibu: Swalah yako ni sahihi – Allaah akitaka. Kwa kuwa ulikuwa hujabainikiwa na makatazo juu ya hili. Kwa hiyo swalah yako ni sahihi – Allaah akitaka. Lakini usiswali ndani yake baada ya kubainikiwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (10) http://alfawzan.af.org.sa/node/2053
  • Imechapishwa: 03/02/2017