Ameswali kwa kukaa chini nyuma ya imamu ilihali anaweza kusimama

Swali: Nilikuwa nikiswali nyuma ya imamu kisha mtoto akalia kilio kikali jambo ambalo liliwashawishi waswaliji, jambo ambalo lilinilazimisha kuswali Rak´ah kwa kuketi chini. Baada ya kumaliza kuswali akaninasihi maamuma mmoja kuirudi swalah yangu kwa sababu nimekwenda kinyume na imamu. Je, aliyosema ni sahihi?

Jibu: Ndio. Mwenye kukaa katika swalah ya faradhi ilihali anaweza kuswali kwa kusimama swalah imebatilika. Ni lazima kwake kuirudi. Hata kama mtoto atalia. Mwache alie na hakuna neno.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ad-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/3712/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D9%85%D9%86-%D8%B5%D9%84%D9%89-%D8%AC%D8%A7%D9%84%D8%B3%D8%A7-%D8%AE%D9%84%D9%81-%D8%A7%D9%84%D8%A7%D9%85%D8%A7%D9%85-%D8%AF%D9%88%D9%86-%D8%B9%D8%B0%D8%B1
  • Imechapishwa: 19/04/2020