Ameswali Dhuhr kwenye uwanja wa ndege kabla ya kuingia wakati

Swali: Nilikuwa kwenye uwanja wa ndege hali ya kuwa ni msafiri. Nikaona kundi linaloswali Dhuhr na nikajiunga nao. Baada ya kumaliza kuswali Dhuhr wakakimu ili waswali ´Aswr. Walipokuwa wanakimu nikasikia adhaana ya Dhuhr. Nikaingiwa na kitu ndani ya nafsi yangu lakini hata hivyo nikawa nimeswali nao ´Aswr na baada ya hapo nikaswali Dhuhr na mkusanyiko mwingine badala ya ile swalah ya kwanza. Kitendo changu ni sahihi?

Jibu. Ndio wajibu wako. Dhuhr haisihi kabla ya kuingia kwa wakati. Ilikuwa ni wajibu kwako vilevile kuwazindua ili wazirudi swalah zao. Swalah haisihi kabla ya kuingia wakati wake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (10) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-08-13.mp3
  • Imechapishwa: 07/06/2020