Ameshindwa kutekeleza nadhiri ya kuchinja kila mwaka


Swali: Mwenye kuweka nadhiri ya kuchinja kila mwaka lakini baadhi ya miaka akashindwa. Ni kipi kinachomlazimu?

Jibu: Anatakiwa kutoa kafara ya kiapo chake. Kafara ya nadhiri inayovunjwa inakafiriwa kafara ya kiapo, kama ilivyotajwa kwenye Hadiyth.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (105) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/20-03-1441-H-%20igah.mp3
  • Imechapishwa: 22/11/2020