Ameshindwa kufunga siku kumi za Dhul-Hijjah kwa sababu ya udhuru

Swali: Kuna mwanamke ambaye ni mtumzima ambaye anafunga yale masiku kumi ya Dhul-Hijjah daima katika kila mwaka isipokuwa tu mwaka huu ambapo anasema kwamba yeye atafunga siku tatu tu au nne. Je, inafaa kwake kufanya hivo?

Jibu: Mwanamke huyu ambaye alikuwa na mazowea ya kufunga siku kumi za mwanzo za mwezi wa Dhul-Hijjah na katika mwaka huu kuna jambo ambalo limemzuia katika maradhi, kuchoka, amekuwa mzee sana na mfano wa hayo tunamwambia: kufunga swawm za sunnah sio jambo la wazima kwa mtu walau atakuwa na afya njema. Kwa mfano mtu ana mazowea ya kufunga masiku matatu meupe na katika mwezi huu akawa hakuweza au akasikia uvivu kuyafunga, hakuna neno kwake kuyaacha kwa sababu yamependekezwa tu. Lakini mtu akiacha sunnah hii kwa sababu ya udhuru basi anaandikiwa thawabu zake. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mja akiumwa au akasafiri basi huandikiwa yale aliyokuwa akifanya pindi alipokuwa mkazi na mwenye afya nzuri.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawa (20/46)
  • Imechapishwa: 13/08/2018