Swali: Kuna mtu alifunga katika Ramadhaan akashikwa na kiu kwelikweli ambapo akanywa maji. Ni ipi hukumu?

Jibu: Ni wajibu kwake kulipa na wala hatotoa kafara kwa mujibu wa maoni sahihi zaidi ya wanachuoni. Ikiwa alichukulia hilo wepesi basi ni wajibu kwake kutubu kwa Allaah pamoja vilevile na kulipa [siku hiyo]. Kuhusu kutoa kafara si wajibu isipokuwa tu kwa yule ambaye amefanya jimaa mchana wa Ramadhaan miongoni mwa wale ambao wanawajibika kufunga. Hadiyth zimepokelewa juu ya hilo tu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.ajurry.com/vb/showthread.php?t=2436
  • Imechapishwa: 23/05/2018