Swali: Ni ipi hukumu mswaliji akiswali swalah ya Maghrib na akasahau Tashahhud ya mwisho?

Jibu: Mtu akisahau Tashahhud ya mwisho katika swalah ya Maghrib au nyingine basi anatakiwa kurudi katika kitako chake na alete Tashahhud ya mwisho kisha asujudu Sujuud ya kusahau na atoe salamu. Vilevile anaweza kutoa salamu kisha akasujudu Sujuud ya kusahau. Akitaka atasujudu Sujuud ya kusahau kabla yake au baada yake. Bora afanye hivo baada ya salamu. Kwa sababu ametoa salamu kwa kupunguza. Kama amesahau Tashahhud ya mwisho ambapo akatoa salamu basi anatakiwa kurudi ndani ya swalah yake ikiwa kitambo si kirefu…

Lakini ikiwa kumepita kitambo kirefu anatakiwa kuianza swalah yake mwanzo. Ikiwa kumeshapita kitambo kirefu kwa mujibu wa desturi, basi atairudia swalah yake mwanzo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3707/حكم-من-نسي-التشهد-الاخير-في-الصلاة
  • Imechapishwa: 06/06/2022