Amesahau kunyoa kichwa chake baada ya Sa´y

Swali: Kuna mtu amefanya ´Umrah na akasahau kunyoa kichwa chake baada ya kufanya Twawaaf na Sa´y ambapo akavaa nguo zake za kawaida. Baadaye akakumbuka kuwa alisahau kunyoa kichwa. Ni kipi kinachomlazimu hivi sasa?

Jibu: Pale alipokumbuka ndipo analazimika kuvua nguo zake, kuvaa mavazi ya Ihraam na kunyoa kichwa chake. Halafu ndio avae nguo zake za kawaida.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (21) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Umdah-13-2-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 08/03/2020