Swali: Ipi hukumu ya mwanamke ambaye ni wajibu kwake kulipa baadhi ya siku katika Ramadhaan. Ramadhaan iliopita alisahau kulipa mpaka hivi sasa.

Jibu: Ikimjia Ramadhaan ya pili, ataifunga. Kisha atalipa baada ya Ramadhaan na atalisha maskini pamoja na kila siku kulipa, kwa kuwa alichelewesha kulipa zaidi ya mwaka bila ya udhuru.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wasswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://alwasabi.al3ilm.com/alfatawaa
  • Imechapishwa: 10/05/2020